Exodus 16:23-28

23 aMusa akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Bwana. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”

24Kwa hiyo wakavihifadhi mpaka asubuhi, kama Musa alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. 25Musa akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Bwana. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. 26 bKwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwepo chochote.”

27Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. 28 cNdipo Bwana akamwambia Musa, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini?
Copyright information for SwhKC